Kocha mkuu wa Coastal Union amesema ameridhishwa na maendeleo ya timu yake tangu kuanza kwa msimu huu. Ameeleza kuwa vijana wanaonesha nidhamu na kujituma.

Katika mazoezi ya hivi karibuni, kocha alisisitiza umuhimu wa kumalizia nafasi wanazopata ili kuongeza idadi ya mabao.

Aidha, aliwahakikishia mashabiki kuwa timu itaendelea kupambana ili kufikia malengo ya msimu.