Mashabiki wa Coastal Union walijitokeza kwa wingi katika mchezo wa nyumbani uliochezwa Mkwakwani. Hali hiyo iliongeza morali kwa wachezaji uwanjani.
Kuanzia dakika za mwanzo, mashabiki walikuwa wakishangilia na kuimba nyimbo mbalimbali za kuisapoti timu yao.
Uongozi wa klabu umeishukuru jamii kwa kuendelea kuiunga mkono timu katika nyakati zote.